Imamu Mkuu Ampokea Gavan awa Wilaya ya Borno, Nigeria

Taarifa imefasiriwa na Bw., Said Moshtohry

  • | Wednesday, 19 February, 2025
Imamu Mkuu Ampokea Gavan awa Wilaya ya Borno, Nigeria

 

Sheikh wa Al-Azhar Ampokea Gavana wa “Jimbo la Borno, Nigeria”,ili kujadili njia za ushirikiano katika nyanja za mawaidha na Elimu

Gavana wa Borno Apongeza Juhudi za Imam Mkuu katika kuimarisha maadili ya kuishi pamoja baina ya wananchi

Leo Jumatatu, Mheshimiwa profesa Ahmed Al-Tayyeb, Sheikh wa Al-Azhar, amempokea bwana Babagana Zulum, Gavana wa “Jimbo la Borno” nchini Nigeria, akifuatana na ujumbe wa wahusika wa jimbo hilo waliomaliza masomo yao katika Al-Azhar, ili kujadili njia za msaada wa Al-Azhar kwa wana na maimamu wa Borno katika nyanja za mawaidha na elimu.

Sheikh wa Al-Azhar alisisitiza kwamba taasisi hiyo inashughulika kwa kuwasaidia waislamu nchini Nigeria; kupitia kutuma misafara ya kielimu na kimawaidha, kuwapokea wanafunzi wa Nigeria ili kusoma katika Al-Azhar, na kuwapa ufadhili wa masomo, hasa wanafunzi wa Nigeria, na alieleza kuwa Al-Azhar inakusanya zaidi ya wanafunzi 5,000 wa Nigeria katika ngazi tofauti za kielimu, na inatoa ufadhili wa masomo 55 kila mwaka kwa wanafunzi wa Nigeria, pia inatuma maimamu 12 kwa Nigeria ili kueneza maadili ya wastani na msimamo wa kati.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Babagana Zulum alielezea furaha yake kwa kukutana na Sheikh wa Al-Azhar, akisifu juhudi zake katika kuimarisha maadili ya usamehevu na kuishi kwa amani kati ya jamii mbalimbali, na jukumu ya Al-Azhar katika kuunga mkono elimu na kueneza Daa،wa ya kiislamu nchini Nigeria, akibainisha kuwa Jimbo la Borno lina shule ya ya Al-Azhar iliyoanzishwa mwaka 1991, ambayo inawahudumia idadi kubwa ya wanafunzi wa kike na wa kiume, jambo lilichangia katika kuimarisha utamaduni wa kiislamu na kuimarisha mtaala kati wa Al-Azhar katika jimbo.

Gavana wa Borno alisisitiza kuwa nchi yake inatarajia kupanua njia za ushirikiano pamoja na Al-Azhar, na kuongeza idadi ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Nigeria, pamoja na kufaidika na programu za mafunzo kwa maimamu wa Borno katika Chuo cha Kimataifa cha Al-Azhar cha mafunzo ya maimamu, ili kuwalinda vijana dhidi ya fikra kali na kufaidika na ujuzi wa Al-Azhar katika kueneza maadili ya kati na kuimarisha dhana za usamehevu kati kati ya wananchi wa Nigeria.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.