🔵 Kwanza: Kuhusu kuimarisha nafasi ya vijana katika kazi za kiraia na za kijamii kwa ujumla, jukwaa linapendekeza yafuatayo:
* Kuandaa programu za mafunzo kwa vijana kuhusu ujuzi wa kazi za kijamii, uongozi na ubunifu.
* Kusaidia miradi ya vijana inayolenga kushughulikia changamoto za kijamii na kiuchumi katika jamii za mitaa.
* Kutoa msaada wa kifedha na kiteknolojia kwa mashirika ya kiraia yanayofanya kazi ya kuwawezesha vijana, na kuhamasisha mashirika hayo kuwajumuisha vijana katika miradi yao ya kijamii.
* Kuanzisha mitandao ya mawasiliano na ushirikiano kati ya mashirika ya kiraia na taasisi za serikali zinazoshughulikia masuala ya vijana kama vile Wizara ya Vijana na Michezo, Wizara ya Elimu na Chuo Kikuu cha Al-Azhar ili kuwahusisha vijana katika miradi na shughuli mbalimbali za ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa.
* Kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za elimu na mashirika ya kiraia ili kuandaa programu za kielimu zinazohamasisha fikra za kina, kukuza dhana ya uraia wa kuwajibika kwa vijana, na kuwalinda dhidi ya fikra kali huku wakihamasishwa kushiriki kwa njia chanya katika jamii.
* Kuwasihi vijana wa nchi yetu kuhakikisha kuwa wanathibitisha kwamba taarifa na habari wanazozipokea kupitia vyanzo rasmi, kulingana na kauli ya Mwenyezi Mungu: "Basi chunguzeni..."
🔵 Pili: Kuhusu kuimarisha nafasi ya vijana katika kuunga mkono suala la Palestina:
* Kulijumuhishe suala la Palestina katika mitaala ya elimu katika ngazi mbalimbali, kwa kutilia mkazo vipengele vya kihistoria, kibinadamu na kisheria vya suala hilo, na kuonyesha nafasi muhimu ya Misri hasa Al-Azhar katika kulitetea suala hilo. Hii itasaidia kukuza uelewa wa vijana kuhusu haki za watu wa Palestina na kuimarisha msaada wao wa dhati kwa ajili ya haki hiyo kupitia majukwaa ya kidijitali.
* Kuanzishwa kwa mfuko wa kusaidia vyombo mbadala vya habari vya vijana, kama silaha madhubuti inayowasilisha maudhui chanya na ya kujenga, yanayoshughulikia masuala ya kijamii na kibinadamu kwa uelewa na uwajibikaji. Mfuko huu utatoa jukwaa la kuvutia na la kuaminika kwa vijana kuonyesha mawazo na ubunifu wao, na kuwalinda dhidi ya sumu ya vyombo vya habari vyenye msimamo mkali au upendeleo wa baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa dhidi ya haki ya kuanzishwa kwa taifa la Palestina.
* Kuanzisha kampeni kubwa ya kidijitali, kwa ushiriki wa vijana, inayolenga kufichua unyama wa uvamizi wa Kizayuni na kutoa uelewa kwa jamii ya kimataifa kuhusu haki za watu wa Palestina. Kampeni hiyo itumie mbinu za kisasa ili kufikia hadhira kubwa zaidi duniani.
🟦🟦 Kwa ajili ya hilo, Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra potofu kinasisitiza umuhimu wa kuendeleza ujuzi wa vijana katika matumizi ya vyombo vya habari vya kidijitali kwa njia zifuatazo:
- Kuandaa warsha na kozi za mafunzo kwa vijana kuhusu ujuzi wa vyombo vya habari vya kidijitali, kukabiliana na hotuba za chuki na fikra kali, ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa maudhui, masoko ya kidijitali, na mawasiliano ya ufanisi. Katika hili, Kituo cha Al-Azhar kitatangaza hivi karibuni kuhusu mkoba wake wa mafunzo ambao utakuwa msingi wa mafunzo ya Al-Azhar katika kuvunja fikra potofu katika muktadha wa Kiarabu na wa Kimagharibi.
- Kusaidia miradi ya vijana inayotumia vyombo vya habari vya kidijitali kupambana na habari za uongo na hotuba za chuki. Kituo kiko tayari kushirikiana na mawazo yoyote yenye manufaa katika suala hili.
- Kutoa majukwaa kwa vijana kuonyesha ubunifu wao wa kidijitali na kubadilishana uzoefu. Kituo kimetangaza kuzinduliwa kwa jukwaa la “Ihyaa” kama mwanzo wa majukwaa mengine ya kuwasiliana na vijana.
*** Kwa kumalizia, jukwaa la "Sikiliza na Zungumza" katika toleo lake la nne linasisitiza umuhimu mkubwa wa kutekeleza mapendekezo haya kwa vitendo, na linatoa wito kwa taasisi zote zinazohusika pamoja na vijana wenye maono kushirikiana na kushikamana kufanikisha malengo yaliyokusudiwa, kwa kuamini kuwa vijana wetu ni viongozi wa kesho na waasisi wa mustakabali. Tunakaribisha kwa moyo wote mapendekezo na miradi mbalimbali, hasa katika maandalizi ya toleo la tano la jukwaa hili katika mwaka ujao, Inshaa Allah.