Imefasiriwa na Bw., Farid Mohammed
Wakati wa mabadiliko ya haraka yanayotokea katika ulimwengu wa kisasa, suala la kuporomoka kwa maadili linaonekana kama moja ya matukio hatari ambayo yanatishia muundo wa jamii na utulivu wake, Hasa katika jamii za Waarabu na za Kiislamu ambazo daima zimekuwa na sifa ya utamaduni na maadili yaliyowekwa katika dhamiri zao za pamoja, alama za Kuporomoka huku hazijafichika tena, lakini yamekuwa sehemu ya mandhari ya kila siku katika mazingira mengi, iwe kupitia maneno ya kawaida, au kupitia mahusiano ya kijamii yaliyovunjika, au mifumo ya tabia isiyodhibitiwa, Hapa, roli ya Kituo cha cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali inadhihiri katika kukabiliana na jambo hili hatari kutoka kwa mtazamo wa uchambuzi, katika jaribio la kutoa matibabu ya kielimu ya kina ambayo huweka mikono ya wale wanaohusika juu ya mapungufu na njia za mageuzi.
Imeonekana kuenea kwa tabia ambazo ni ngeni kwa mfumo wa maadili halisi, kama vile: uwongo, unafiki, udanganyifu, na Ukiukaji wa kimatusi na wa kimwili, na kupungua kwa heshima kati ya wanajamii, Mbali na utawala wa ubinafsi na wa kimada badala ya roho ya jamaa na mshikamano wa kijamii, na linalofanya mambo kuwa magumu zaidi ni kwamba tabia hizi hazichochea tena hisia za kutokubalika kwa umma kama zilivyokuwa zinafanya hapo awali, lakini, nyakati fulani hufafanuliwa au kukubaliwa kama “jambo halisi,”au “njia ya kubakia,” au “kupatana na mabadiliko ya nyakati,” jambo ambalo huonyesha mabadiliko makubwa katika ufahamu wa jamii na kushuka kwa mamlaka ya dhamiri ya pamoja.
Mfumo wa maadili kati ya zamani na sasa
Mfumo wa maadili katika jamii za wanadamu haujakuwa thabiti kupitia zamani, bali daima ulikuwa katika hali ya nishati na maendeleo, ikiakisi asili ya muktadha wa kitamaduni, kijamii na kisiasa inayoizingira, Wakati wa kulinganisha kati ya zamani na sasa, kiwango cha mabadiliko ambacho kimetokea katika mfumo huu kinabainika wazi, iwe katika kiwango cha kubaki, unishati, au vipaumbele.
Hapo awali, maadili yalikuwa thabiti kwa asilimia fulani; ambapo yalipitishwa kwa vizazi kupitia njia wazi kama vile: familia, elimu ya kidini, na jamii ya kijad, na yalikubaliwa sana bila mashaka mengi, Maadili kama vile: “ukweli, uaminifu, haya, kuwaamilia wazazi kwa wema, kuwaheshima wazee, uadilifu, na utimizo wa ahadi” yaliwakilisha kanuni thabiti katika dhamiri ya pamoja, na Inaunda msingi wa tabia ya mtu binafsi na ya kikundi, udhibiti wa maadili ulikuwa kiwango cha hadhi ya kijamii na heshima ya kijamii, jambo ambalo liliimarisha mshikamano kati ya wanajamii na kupunguza alama ya kupotoka au kutengana.
hivi sasa, maadili yameshuhudia mabadiliko ya haraka na magumu kutokana na sababu nyingi, yenye umaarufu zaidi kati yao ni: utandawazi, uwazi wa vyombo vya habari, maendeleo ya kiteknolojia, na kuzorota kwa baadhi ya mifumo ya kimalezi ya kijadi, Leo, mtu anakabiliwa na mivuto mengi tofauti ya kimaadili ambayo mara nyingi zinazokinzana, Ambalo lilisababisha hali ya kuchanganyikiwa au kupoteza maadili, na yamezuka maadili mapya ya kimada na ya mtu binafsi kama vile: mafanikio ya mtu binafsi kwa njia yoyote, kujitambua kwa kutengwa na kikundi, na sura ya kijamii, kwa gharama ya maadili halisi ya pamoja kama vile kujitolea, kujinasibu na kuheshimiana.
Sababu ya Kuporomoka kwa mfumo wa maadili
Kuna sababu nyingi zilizochangia kufikia hatua hii ya kuzorota kwa maadili, Labda jambo kuu zaidi kati ya haya ni kupunguka kwa roli ya familia katika malezi, kwa sababu ya kukosea kwa wazazi au kutokuwepo kwa rowaza njema, Ambayo huwaacha watoto katika hatari ya ushawishi wa nje ambao hauzingatii mipaka ya jamii, pia Baadhi ya vyombo vya habari, hasa vile vinavyotafuta msisimko na faida ya haraka, vilichangia hasi katika kukuza wanamitindo wa kijuujuu au potovu ambao hutawala hadharani licha ya kukosa thamani yoyote au ukweli au ubinadamu.
Mitandao ya kijamii haikuepushwa kuhusika katika anguko hilo, Badala yake, bali ilikuwa na ushawishi mkubwa zaidi, Ilitoa nafasi wazi kwa usambazaji wa mawazo na tabia bila vidhibiti wala vikwazo, Ilichangia kusambaza aina ya kujisifu, kuiga kipofu, na kuasi juu ya maadili, chini ya kauli mbiu: “Uhuru wa kibinafsi”, Kwa kutokuwepo karibu kabisa kwa muamko wa kuhakiki au wajibu wa kitabia. Wakati huo huo, ushawishi wa taasisi za kielimu na za kidini ulipungua katika kupanda maadili na kuyaimarisha, kama matokeo ya kuzingatia pande ya sura au ya utambuzi, bila kuzingatia kwa kweli kwa mwelekeo wa kihisia na kimalezi, Ambayo ilichangia kuzalisha vizazi vinavyojua mengi, lakini havijisikii kujinasibu au kujilazimika kwa maadili.
Haiwezikani kulipuuza Jukumu la migogoro ya kiuchumi na ya kijamii katika muktadha huu; ambapo Mateso ya watu binafsi kutokana na shinikizo la maisha, kupunguka kwa uadilifu wa kijamii, na kukosekana kwa fursa sawa ni vitendakazi ambavyo vinaunda mazingira yenye rutuba ya kukata tamaa na kuzaa tabia zisizo za kijamii, ambazo watu hushughulikia na maadili kama anasa zisizo na maana.
Pia Imani dhaifu katika taasisi na kutokuwepo kwa watu wa kuigwa katika nafasi za uwajibikaji huimarisha imani hiyo - ingawa ni imani potofu - kwamba kufuata maadili hakuleti manufaa, wakati ambapo fursa na ulaghai vinaweza kufungua milango ya mafanikio ya uwongo.
Njia ya Kutibu kuporomoka kwa mfumo wa maadili:
Lakini ingawa ugumu wa tukio, uwezekano wa mageuzi bado upo, na hata muhimu, na matibabu huanza kutoka ndani ya familia, Familia, ambayo lazima irejeshe jukumu lake kama ngome ya kielimu, inasisitiza maadili ndani ya mtoto tangu umri mdogo, kupitia mfano mzuri, mazungumzo ya kufahamiana, na uangalizi mzuri, Wakati huo huo, vyombo vya habari lazima vibebe wajibuake katika kuzalisha mada bora ambayo inaimarisha maadili, na kusambaza mifano chanya, badala ya kumfanya mwanadamu kama bidhaa na kupuuza ufahamu.
Kuhusu taasisi za kielimu, lazima ziangalie upya mitaala na mbinu zao, ili malezi ya kimaadili iwe sehemu muhimu ya mchakato wa elimu kupitia mitaala, shughuli na tabia ya jumla ndani ya shule na chuo kikuu, yanapaswa pia kuanzisha Mazungumzo ya wastani ya kidini, ambayo huzingatia ufahamu sahihi wa dini, ambayo pia huunganisha imani na tabia, na hukadimisha maadili makuu ya Kiislamu kama vile uadilifu, huruma, uaminifu na ukweli kama kiini cha dini, sio tu kauli mbiu zinazokaririwa.
Katika muktadha huu, roli ya Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra kali inazuka kama mimbari madhubuti ya kisayansi na kifikra inayojitahidi kufichua upotovu wa kiakili na kitabia, na kukadimisha muono uliostaarabika wa Uislamu, ambamo maarifa yanaunganishwa na maadili, na ambamo wajibu wa kidini unaingiliana na hisia za mwanadamu. Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra kali kina nia ya kuzalisha mada ya kukuza ufahamu na ya kuelimisha ambayo yanaelekeza vijana kwenye maadili ya kujinasibu, heshima na uwazi unaohisabiwa mbali na kutia chumvi au uzembe.
Kwa hivyo, opresheni ya kutibu kuporomoka kwa maadili sio jukumu la upande mmoja, lakini ni jukumu la pamoja ambalo linahitaji juhudi za pamoja za familia, shule, taasisi za kidini, vyombo vya habari na mashirika ya kiraia, ili kuunda mradi wa kitaifa wa maadili ambao humjenga tena mwanadamu, na kulinda jamii kutoka ndani, na kuilinda dhidi ya kila aina ya upotovu na msimamo mkali. Hakika mchakato wa kumjenga mwanadamu na kutengeneza ufahamu wa pamoja ni mchakato mgumu na mpana jinsi ulivyo, lakini unabaki kuwa njia pekee ya kuokoa ulimwengu kutoka kwenye dimbwi la mawazo na tabia potovu zinazokataliwa na akili timamu na kukataliwa na dhamiri zilizoamshwa.