Ghaza Mpya… mji mpya ama ni Jela Kubwa

Ghaza Mpya… mji mpya ama ni Jela Kubwa

  • | Thursday, 17 July, 2025
Ghaza Mpya… mji mpya ama ni Jela Kubwa

Makala hii imeandaliwa na kitengo cha Lugha ya Kiheberu

Imefasiriwa na Bw. Farid Mohammed Farid

 

     Katika hatua ambayo ina taathira kubwa za kibinadamu na kisiasa kwa mustakbali wa Ukanda wa Ghaza uliopoteza maisha, magazeti kadhaa ya Kiebrania yamefichua mpango uliotayarishwa na utawala wa Kizayuni wa kuanzisha eneo jipya kwenye magofu ya mji wa Palestina wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Ghaza, ili kiwe kituo kikuu cha mkusanyiko wa wakazi wa Ghaza; ambapo Wapalestina wanazuiliwa ndani yake baada ya kufanyiwa ukaguzi wa usalama, huku wakiwa hawaruhusiwi kuondoka tena kamwe.

Licha ya majaribio ya utawala wa Kizayuni ya kudhihirisha mpango wake ovu katika picha ya mradi wa kibinadamu kwa kulipatia eneo hili jina linalodaiwa kuwa "Mji wa Kibinadamu," lakini vifungu  vyake vinathibitisha bila shaka yoyote kwamba uvamizi huo kwa hakika unalenga kuanzisha jela kubwa ndani ya Ukanda wa Ghaza; Kwa mujibu wa kile kilichoelezwa kwenye tovuti hizo, mpango huo wa kizayuni unajumuisha vifungu kadhaa, kama ifuatavyo:

  • Kuingiza Wapalestina 600,000 katika eneo hili jipya katika awamu ya kwanza baada ya kuwaweka katika ukaguzi mkali wa usalama.
  • Kutoruhusiwa kuondoka katika eneo hili, au kutoka nje yake mara tena.
  • Ilikubaliwa kuanzisha eneo hilo kati ya mhimili wa Salah Al-Din (Philadelphia) na Morag, kusini mwa Ukanda wa Ghaza.
  • utawala wa Kizayuni unadhibiti kikamilifu katika kuingiza kwa chakula na misaada ya kibinadamu kwenye eneo hilo.
  • utawala wa Kizayuni unazingatia kuanzishwa kwa gereza hili kubwa kuwa moja ya misingi ya kile wanachokiita: "siku iliyofuatia" vita vya maangamizi huko Ghaza.
  • Uvamizi huo unachukua fursa ya siku 60 zinazotarajiwa kusitisha vita vya maangamizi huko Ghaza ili  kuanzisha eneo hili.
  • Kuanzisha vituo 4 vipya vya usambazaji wa misaada vinavyosimamiwa na kile kiitwacho "taasisi ya Ghaza ya kibinadamu" inayoungwa mkono na Marekani na utawala wa Kizayuni.
  • Kuanzishwa kwa eneo hili ni muhula wa kwanza wa mpango wa kuwaondoa Wapalestina kutoka Ghaza hadi katika nchi nyingine kadhaa; ambapo Baadhi ya ripoti zilieleza kuwa mawasiliano ya awali tayari yamefanyika na nchi kadhaa duniani bila kutaja majina yao.

Katika taarifa yake inayofichua mwelekeo wa kina wa kimkakati, Waziri wa Vita wa Kizayuni, Yisrael Katz, alionyesha kwamba kuna hamu inayoongezeka ndani ya utawala wa Kizayuni wa kuhimiza kile alichokiita "uhamiaji wa hiari" wa watu wa Ghaza. Ameashiria kuwa Waziri Mkuu wa Uvamizi huo, Benjamin Netanyahu, anafanya kazi ya kubainisha nchi ambazo zinaweza kukubali kuwapokea watu wa Ghaza, ndani ya mpango wa kizayuni wa kuwaeneza Wapalestina nje ya mipaka ya Ukanda wa Ghaza.

Waziri huyo wa Kizayuni pia ameeleza kuwa vikosi vya kizayuni vitalinda eneo ambalo mji huo wa kibinadamu umepangwa kuanzishwa kusini mwa Ukanda wa Ghaza, lakini havitachukua usimamizi wake wa moja kwa moja, wala hawatasimamia usambazaji wa misaada. Ameongeza kuwa utawala wa Kizayuni unataka kushirikisha vyombo vya kimataifa katika mradi huu, katika jaribio la kuupa mpango huo bima ya kimataifa; Ili kupunguza ukosoaji unaotarajiwa.

Kipengele chenye utata zaidi cha mpango huu kinajitokeza katika muhula unaofuata; ambapo Idhaa ya Kiebrania 12 ilifichua kwamba uvamizi huo unafanya kazi ili kuwezesha mifumo mingi ili kuharakisha kile ilichokiita: "uhamiaji wa hiari" kwa watu Wa Ghaza baada ya kuwakusanya ndani ya eneo lililopendekezwa. Akibainisha kuwa jeshi la uvamizi kwa hakika limeanza kuweka misingi ya utekelezaji wa mpango kimatendo, katika tukio ambalo linatahadharisha mabadiliko makubwa katika ramani ya kiwakazi.

Kituo cha Alazhar cha kupambana na fikra kali kinathibitisha kwamba mpango huu mbaya si chochote ila ni jela ya ubinadamu nyuma ya waya, na uuzaji wa uhamiaji kutoka mizizi kama suluhisho wa milele, na kwamba lengo lake ni kuwadhalilisha zaidi na kuwatia njaa Wapalestina, kuunda mazingira bora ya kulazimishwa kukimbia, na kuwaondoa watu wa Ukanda wa Ghaza; nao Ndio lengo kuu la Wazayuni tangu kuanza kwa vita vya maangamizi mwezi Oktoba 2023, na mpango huu unafanikisha malengo ya Wazayuni ya kuikalia kwa mabavu ardhi yote ya Palestina na kuwang'oa Wapalestina kutoka ardhi yao ya kihistoria.

 

Kwa kweli, ni vigumu kwetu kuelewa uwezo wa uvamizi wa kujisifu wakati wa kulipatia istilshi ya "uhamiaji wa hiari" linatumiwa kama chaguo la ukarimu, na hatujui jinsi ya kuwa "uhamiaji wa hiari" chini ya kuzingirwa, njaa, na uharibifu kamili wa aina zote za maisha. Inawezaje kuwa "kwa hiari" juu ya mabaki ya mashahidi zaidi ya 50,000, juu ya magofu ya ukanda ulioharibiwa kabisa, na kwa gharama ya kuhamisha na kuwatia njaa karibu watu milioni mbili; Kukimbia hapa sio chaguo la hiari, lakini ni aina ya kuokoka kutoka kwa kuzimu ya uvamizi ambao historia haijawahi Kujua mfano wake hapo awali.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.