Uislamu Hujali Mahitaji ya Roho na Mwili

Uislamu Hujali Mahitaji ya Roho na Mwili

Imeandaliwa na Dkt. Alaa Salah Abdulwahed

  • | Monday, 22 September, 2025
Uislamu Hujali Mahitaji ya Roho na Mwili
Dini ya Uislamu imekuja kwa wito inayotokana na maumbile ya kibinadamu, kwa hivyo, sheria ya dini hiyo inazingatia kwa kiasi kikubwa mahitaji ya roho na mwili wa mwislamu, ambapo sheria hiyo imekusanya kanuni za kupanga maisha nzima ya mwanadamu na kuangalia mahitaji yake ya kiroho na ya kimwili. Mwenyezi Mungu (S.W.) Amebainisha kuwa mwanadamu anatakiwa kuhakikisha kuwa anajitosheleza kiroho na kimwili ili awe anaenda sambamba na hikima yake (S.W.) Aliyesema: {Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaaziya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawefanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi.Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi} Qasas: 77.
Kwa hakika ujumbe wa Mtume (S.A.W.) una dhamira mbalimbali miongoni mwa dhamira hizo, kuhimiza tabia njema na kuzitakasa nafsi na kuzitaharisha kutoka madhambi na maovu yaliyo dhahiri na yasiyo dhahiri. Kwa hivyo Mtume alijumlisha malengo ya utume wake kwa kusema: "Kwa kweli nimepewa utume kwa ajili ya kutimiza tabia njema". Qurani Takatifu imebainisha hali hii ikisisitiza kuwa wasialmu wote wanatakwa kumfuata Mtume wao kutekelea malengo haya na dhamira hizi.
Mwenyezi Mungu Alielezea lengo la kutumwa kwa Mtume Aliposema: {Ewe Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na awafundishe Kitabu nahikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima} [2/129], na Alisema pia: {Kama tulivyo mtuma Mtume kwenu anaye tokana nanyinyi, anakusomeeni Aya zetu na kukutakaseni na kukufundisheni Kitabu na hikima na kukufundisheni mliyo kuwa hamyajui} [2/151] na katika sura nyingine Alisema (S.W.): {Hakika Mwenyezi Mungu amewafanyia wema mkubwaWaumini vile alivyo waletea Mtume aliye miongoni mwaowenyewe, anaye wasomea Aya zake, na anawatakasa, na anawafunza Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya hapowalikuwa katika upotovu ulio wazi} [3/164].
Na kwa kueleza sababu kuu ya utume wa Mtume, Mwenyezi Mungu Alisisitiza hayo kwa kusema: { Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasiojua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, naawafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri * Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao. Na Yeyendiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima} [62/2-3].
Imamu Al-Twabariy katika kueleza maana ya aya hii katika tafsiri yake alisema kuwa maana inayokusudiwa ni kuzitakasa na kuzitaharisha nafsi zao kwa kuwazuia na kuwakataza kuabudu masanamu na kufanya maovu waliyokuwa wanayafanya kabla ya utume wake, kwani kutakasa nafsi inamaanisha kuiokoa na kuisafisha kutokana mabaya yote na kwa watu wa enzi ile ushirikina na maovu mengine mengi yalikuwa yameenea sana wakati ule. Wanavyouni na wataalamu wa tafsiri walekubaliana juu ya kwamba kutaja ushirikina na kufr kama mfano wa maovu na mabaya yaliyokuwa yakifanywa zama hizi ni kwa sababu yalikuwa ndiyo madhambi makuu yaliyokuwa yakiongoza maovu mengine.
Tukiangalia historia ya maisha ya Mtume (S.A.W.) tutaelewa kuwa maisha yake yote ilikuwa inafungamana na mafunzo ya Qurani hasa katika tabia yake kwa hiyo Bi Asha (R.A.) alipotaka kusifu tabia ya Mtume alisema: "Tabia ya Mtume ilikuwa Qurani yenyewe". Kwa mujibu wa mfumo huu wa kuimarisha tabia njema na kuhimiza waumini wazingatie tabia hizo Mtume aliweza kuyatatua matatizo yote aliyokuwa nayo na kuwasia wafuasi wake washikamane mfumo huo kwa ajili ya kushinda shida yoyote maishani mwao.
Pia, Mtume alikuwa anawaelekeza maswahaba wake na waislamu kwa jumla kuwa utiifu na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu ndio sababu ya kupambana na mvutano wa mashetani na ushawishi wake, ambapo kulazimika maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu kunamsaidia mwislamu ajiokoe kutokana na maovu na madhambi, kama Alivyosema Mwenyezi Mungu: {Soma uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala.Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwayakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda} [29/45].
Naye Mtume alikuwa anaeleza hivyo hivyo kwa kubainisha kuwa ibada inaitakasa na kutaharisha nafsi kutoka kwa maovu na wasi wasi, kwa hiyo maswahaba walipoeleza shida yao na mmoja aliyekuwa anasali usiku mzima lakini asubuhi anawaibia watu vitu vyao Mtume aliwatuliza kwa kusema: "Swala yake itamzuia uporaji". Ama kuhusu Zaka Mwenyezi Mungu alibainisha pia kuwa inamsaidia mja aitakasa nafsi yake na kutaharisha mali yake kwa kusema: {Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe nauwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombiyako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenyekusikia Mwenye kujua} [9/103].
Hivyo tunaona namna ibada inachangia kuitakasa nafsi na kumsaidia mja ajisafishe roho na kutaharisha nafsi na viungo kutoka maovu yoyote, hali hiyo hiyo inakuwa katika ibada zote Swala, Zaka, Saumu na Hijja.
Vile vile, tunamwona Mtume alivyokuwa anawafundisha maswahaba wake namna ya kuitakasa nafsi na kutubu kutoka madhambi na mabaya katika hali zao zote hata katika wakati wa kijisaidia ambapo Mtume alisema: "Hakika mimi kwenu ni kama baba mlezi, nawafundisheni kama mmoja wenu alikuwa ana haja kubwa basi asielekei Qibla kwa uso wake wala kwa nyuma wala asijisafishe kwa mkono wake wa kulia bali kwa mawe matatu (kufanya Istinjaa)"
Haya yote ni mifano tu ya kubainisha namna Mtume alikuwa na hamu sana kuwasaidia maswahaba na waislamu kwa jumla wazitakasa nafsi na kutaharisha roho na kuwa safi katika hai zao zote.
Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.