Katika miaka ya hivi karibuni, bara la Afrika limekuwa uwanja wa makundi ya kigaidi ambayo yanatumia mbinu dhalimu ili kufanikisha ajenda zao. Moja ya mbinu hizo ni kutumia vibaya wanawake na watoto – makundi mawili yenye udhaifu wa kijamii – kwa njia za unyanyasaji, ukandamizaji na udanganyifu.
Makundi ya kigaidi barani Afrika, hasa )Boko Haram( nchini Nigeria na kundi la )Al-Shabaab( nchini Somalia, yamehusika moja kwa moja katika kuwatumia wanawake kwa malengo mbalimbali, Boko Haram imetekwa wasichana wengi, mfano maarufu ni utekaji wa zaidi ya (wasichana 270 wa Chibok mwaka 2014) walilazimishwa kuolewa na wapiganaji au kutumikwa kama watumwa wa kijinsia.
Bali jambo lililobaya zaidi ni kwamba takwimu kutoka Nigeria zimeonyesha kwamba kati ya mwaka 2014–2018, zaidi ya wanawake na wasichana 150 walitumikwa kama mabomu ya kujitoa mhanga na Boko Haram, wanawake huchaguliwa kwa sababu mara nyingi hawashukiwi na vyombo vya usalama.
Pia Katika baadhi ya maeneo ya Somalia na Kaskazini mwa Kenya, Al-Shabaab wamewatumia wanawake kwenye mitandao ya kijamii kusambaza fikra kali na kuhamasisha uandikishaji wa vijana.
Ama kuhusu watoto katika mikono ya magaidi wameathirika kwa vita vya kigaidi na mara nyingi hutumiwa kama silaha. Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, na Mali, makundi ya kigaidi na waasi wamewahi kuandikisha maelfu ya watoto, wengi hufundishwa kutumia silaha au kufanywa wasaidizi.
Boko Haram imetumia watoto wadogo kubeba mabomu katika masoko au vituo vya usafiri, na mara nyingi watoto hukuzwa kwa fikra kali na kufundishwa kuamini kuwa ugaidi ni "jihad" au "njia ya heshima".
Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba katika Kaskazini mwa Msumbiji, watoto walitekwa, wengine wanalazimishwa kuwa wapiganaji na wasichana kubakwa.
Mambo hayo yaliacha athari za kijamii na kimaendeleo, wanawake na watoto wanapotekwa au kulazimishwa kushiriki vitendo vya kigaidi, familia na jamii hupoteza mshikamano, pia Mashambulizi dhidi ya shule, kama kauli ya Boko Haram “Elimu ya Magharibi ni haramu”, yamesababisha maelfu ya shule kufungwa Kaskazini mwa Nigeria, pia kuna athari za kisaikolojia, wanawake na watoto waliowahi kuwa mateka hubaki na msongo wa mawazo na huzuni ya muda mrefu.
Mifano Halisi Kutoka Afrika
1- Nigeria (Boko Haram): Utekaji wa wasichana wa Chibok 2014, wengine waliuzwa, wengine walilazimishwa kuolewa, na baadhi walitumika kwenye mashambulizi ya kujitoa mhanga.
2- Somalia (Al-Shabaab): Wanawake na watoto hutumika kama wasafirishaji wa silaha na mabomu kutokana na kutoshukiwa sana na askari.
3- Msumbiji: Ripoti za Shirika la Haki za Binadamu zinasema watoto wametekwa na kulazimishwa kujiunga na wanamgambo tangu 2017.
4- Kongo: Watoto huandikishwa kwa nguvu kama wapiganaji, huku wasichana wakifanywa wake wa kulazimishwa.
Njia za Kukabiliana na Tatizo
1- Kuimarisha ulinzi wa wanawake na watoto kupitia sheria na hatua za kimataifa.
2- Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali zinapaswa kusaidia waliopitia ukatili huu kupata msaada wa kisaikolojia na elimu.
3- Kufichua upotofu wa fikra za kigaidi na kuimarisha elimu ya dini na uraia.
Mwishoni, wanawake na watoto wamegeuzwa silaha na makundi ya kigaidi barani Afrika, jambo linalodhalilisha utu na haki za binadamu. Kukomesha hali hii kunahitaji juhudi za pamoja – kitaifa, kikanda na kimataifa – ili kuhakikisha kuwa wale waliolengwa na ugaidi wanapata hifadhi, msaada na mustakabali bora.