Kwa hakika dini ya Uislamu umezingatia sana kufanya bidii na kuwa na uangalifu wa kazi, ukawahimiza waislamu wewe na sifa hiyo. Vile vile Uislamu umetia maanani sana kazi na wafanya kazi, ambapo Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wataviona vitendo vyenu. Kisha mtarudishwa kwa Mjuziwa ya siri na ya dhaahiri; naye atakuambieni mliyokuwa mkiyatenda} [Al-Tawbah: 94], na katika sura hiyo hiyo Mwenyezi Mungu Anawaahidi waumini kuwa kazi zao Yeye Subhana Atazitathmini katika Siku ya Mwisho: {Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhaahiri; naye atakuambieni mliyokuwa mkiyatenda} [Al-Tawbah: 105].
Kwa kuangalia Qurani Tukufu, tunaona kuwa aya nyingi sana zilisisitiza umuhimu wa kuwa na kazi na kujitahidi, sawa katika vitendo vya dunia au vile vya Akhera, ambapo aya hizo takatifu zimekusanya pamoja vitendo vyote vya dunia na Akhera. Zaidi ya hayo, tukiangalia kwa makini kwa aya hizo mbili zilizotajwa juu, tunafahamu kwamba Qurani Takatifu imemtanabahisha mwislamu kuwa Mwenyezi Mungu (S.W.) ndiye mjuzi wa vitendo vyote vya waja wake, na Yeye ndiye Atakaewalipiza vitendo vyao hivyo. Hili kwa lengo la kuwahimiza watu waboresha vitendo vyao na kufanya juhudi zao zote kwa ajili ya kuwa na vitendo bora zaidi na kufanya kazi yake kwa umakini na ufanisi mkubwa.
Miongoni mwa mambo ya msingi kwa kila mwanadamu ambayo anatakiwa kuifanyia kazi kwa bidii na kujitahidi kuyatekeleza ni mchango wake kuiilinda na kuinusuru dini na nchi yake.
Ama kuhusu dini ni uwanja wa kushindana baina ya waumini ambao huwa na hamu kubwa ya kufanikiwa katika masuala ya dini yao kama vile; kutekeleza ibada, kupata radhi ya Mola wao, kuwa na nafasi na mchango mkubwa katika dini yao.
Kuwa na bidii ni sifa mojawapo sifa za waumini wa kweli ambao hawakubali wawe chini wala nyuma ya umma wengine, ambapo muumini anayetaka kufuzu katika dunia kwa mafanikio na ushindi na katika Akhera kwa radhi na malipo mema ya Mwenyezi Mungu huwa na jitihada kubwa kwa ajili ya kuinusuru dini yake, hajui uvivu, madhila, unyonge wala udhaifu katika dini yake.
Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amewaagiza waja wake wafanye kazi kwa bidii na kuunganisha imani na vitendo ambavyo ni kazi kwa kusema katika aya nyingi za Quran Tukufu: {Hakika wale walio amini na wakatenda mema – hakika Sisi hatupotezi ujira wa anaye tenda mema} Al-Kahf-30, na Amesema (S.W.): {Na sema: Tendeni vitendo. Na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini wataviona vitendo vyenu. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhaahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda} Al-Tawbah-105.
Kwa upande mwingine, kuipenda nchi ni sifa mojawapo sifa za kimaumbile wanayo wanadamu wote, kwa hiyo Mtume wetu alishtuka aliposikia kutoka Waraqa bin Noufal kwamba watu wake watamalazimisha ahamie nchi yake kwa kuwa anaipenda sana na amekuwa hataki kuihamia kabisa, na alipokuwa akitoka alisema kauli yake: "Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba Makka ndiko nchi bora zaidi kwa Mwenyezi Mungu na kwangu pia na angalau watu wake wamenilazimisha nihamie nisingetoka hata kidogo"
Na kuipenda nchi si sifa ya wanadamu tu, bali wanyama pia, kwa hiyo si jambo la kushangaza kuwa sheria imekuja kuwahimiza wananchi kuipenda na kuitetea na kupigana kwa ajili yake hata mmoja akipotezwa na maisha yake huwa na fadhila kubwa nayo ni kuwa shahidi aliyekufa kwa ajili ya nchi yake, ambapo shahidi huyu amepewa cheo cha juu kabisa na kutunukiwa na Mwenyezi Mungu na watu pia, Mwenyezi Mungu Amesema: {Wala msiseme kuwa wale walio uwawa katika Njia yaMwenyezi Mungu ni maiti; bali hao ni wahai, lakininyinyi hamtambui} [2/154].
Zaidi ya hayo Mwenyezi Mungu Amewaruhusia wananchi kutangaza upendo wao kwa nchi na kuwa wako tayari kufanya lolot kwa ajili ya nchi hiyo, hata ikiwa ni kupigana na wale wanaotaka kaiharibu nchi na kuwatokeza watu wake kutoka makwao: {Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu,na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu} [60/9].
Wakati huo huo Mwenyezi Mungu Amewaelekeza waumini kuwapenda na kuamiliana na wale wasiofanya uadui wowote dhidi ya nchi kwa wema na uadilifu hata wakiwa si waislamu: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema nauadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [60/8].
Kwa hiyo tunaona kuwa uzalendo na kuipenda nchi katika sheria ndiyo sababu ya kupenda ama kutopenda na chanzo cha kujitolea na kujitahidi kuzuia madhara yoyote dhidi yake nchi tunakotoka. Inafahamika kuwa matini nyingi katika Qurani na Sunna za Mtume zimesisitiza ukweli wa kwamba uzalendo na kuipenda nchi ni sehemu ya imani inayotokana na maumbile ya kibinadamu, na kwamba hisia za upendo kwa nchi ni sifa inayopatikana kwa kila mwenye mwenendo ulio sawa na akili timamu, hata akiwa anaishi nje ya nchi yake hiyo.